You are currently viewing JAY MELODY MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

JAY MELODY MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE MPYA

Msanii wa Bongofleva, Jay Melody amesema albamu yake mpya ambayo ipo mbioni kutoka itakuwa na ngoma 15.

Akizungumza na kipindi cha The Switch ya Wasafi FM,hitmaker huyo wa ngoma ya “Sugar” amesema albamu hiyo aliipanga kuiachia mwaka jana lakini akasogeza mbele ili kujipanga vizuri.

Mbali na hayo, Jay Melody amesema ataachia video ya wimbo wake wa ‘Sugar’ remix aliyomshirikisha Marioo hivi karibuni kwani tayari wamemaliza kushuti video ya wimbo huo.

Utakumbuka Jay Melody anakuwa msanii mwingine kuweka wazi kutoa albamu mwaka huu baada ya Navy Kenzo, Harmonize, Ommy Dimpoz, Marioo, Maua Sama na Zuchu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke