Rapa kutoka Marekani Jay-Z anazidi kutufunulia kurasa za kitabu cha maisha yake kwa kufunguka mengi kuhusu yeye, na sasa ni kurasa ya mitandao ya kijamii.
Kwenye mahojiano ya hivi karibuni na mchekeshaji kevin Hart kupitia podcast ya “Hart to Heart”,Jay-z amefunguka sababu zinazomfanya kutotumia mitandao ya kijamii kwa kile anachodai kuwa mitandao hiyo sio kwaajili yake na sio sehemu ya yeye kujihusisha japo anaamini katika Mageuzi.
“It’s not for me. It’s not for me to engage. I didn’t grow up in that space,” “I believe in evolution so whatever form it is, I accept that”. Amesema Jay Z.
Utakumbuka Jigga anahistoria ya kuingia mara mbili katika mtandao wa Instagram,
Mwaka 2015 alijiunga katika mtandao huo kutoa heshima zake katika kumbukizi ya miaka 57 ya kuzaliwa kwa Marehemu Michael Jackson na 2021 alijiunga tena kuitangaza filamu ya The Harder They Fall.