You are currently viewing JAY Z AJIONDOA INSTAGRAM BAADA YA KUDUMU KWA SAA 24

JAY Z AJIONDOA INSTAGRAM BAADA YA KUDUMU KWA SAA 24

Ni kama Rapa Jay Z hajaona umuhimu wa kuutumia mtandao wa kijamii wa Instagram hii ni baada ya kudumu kwenye mtandao huo kwa chini ya masaa 24 kisha kujiondoa.

Siku ya jana November 3,mwaka wa 2021 Rapa Jay Z alijiunga rasmi na mtandao wa kijamii wa Instagram na kum-follow mke wake Beyonce kisha ku-post picha moja ya cover ya Filamu mpya

Sasa pamoja na kuvuna wafuasi zaidi ya milioni 2 ndani ya masaa 24 Jay Z ameamua kuipotezea akaunt yake hiyo ya Instagram kwa kufuta post alioiweka na kuficha idadi ya watu waliomfuata (followers) na (followng) kwenye mtandao huo.

Jay-Z ni kama alikuwa na lengo la kuitangaza tu filamu yake ya “The Harder They Fall” ambayo amehusika kama mtayarishaji. Filamu hiyo ilioneshwa Jana kwa mara ya kwanza kupitia Jukwaa la Netflix

Mkongwe huyo wa Hip Hop na mfanyabiashara alikuwa sio muumini wa mitandao ya kijamii kabisa, aliwahi kukaririwa akisema; Mitandao ya Kijamii ni mahususi kwa wale ambao hawawezi kujieleza kwenye ulimwengu wa kawaida yaani waoga. Pia ni dunia ya watu ‘fake’ ambao watakuchukia bila sababu kutokana na ukweli kwamba wana mapenzi zaidi kwenye mtindo huu wa maisha kuliko hata binadamu wenzao.

Tovuti ya Billboard inaarifu kwamba Jay-Z aliwahi kujiunga na mtandao wa Instagram mnamo August 29, 2015 na kumtakia heri ya Kuzaliwa marehemu Michael Jackson lakini aliifuta akaunti hiyo ndani ya masaa 14 akiwa tayari amevuna followers Laki moja.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke