You are currently viewing JAY Z AWEKA REKODI YA KUWA MSANII ALIYETAJWA KWENYE VIPENGELE VINGI GRAMMYS

JAY Z AWEKA REKODI YA KUWA MSANII ALIYETAJWA KWENYE VIPENGELE VINGI GRAMMYS

Kwa sasa hakuna zaidi ya Jay-Z kwenye tuzo za Grammy upande wa wasanii waliotajwa mara nyingi zaidi kwenye vipengele vya Tuzo hizo kwa muda wote. Jay-Z amempiku mtayarishaji Quincy Jones ambaye ana nominations 80 kwa kufikisha jumla ya nominations 83.

Hii imekuja baada ya Jigga kutajwa kwenye vipengele vitatu kwenye tuzo za mwaka 2022 ambapo ametajwa kwenye Kolabo ya ngoma ya Bath Salts  aliyoshirikisha DMX na ngoma ya Jail aliyoshirikishwa na Kanye West.

Kipengele cha tatu ametajwa kama mshiriki katika album ya Kanye West DONDA.

Jay-Z ni mshindi mara 23 wa tuzo za Grammy ambazo amewahi kuzichana mara baada ya kushindwa kuibuka na tuzo hata moja mwaka wa 2018 licha ya kutajwa kwenye vipenge vinane.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke