You are currently viewing JAY Z, KANYE WEST & DIDDY WATAJWA KAMA MARAPA WALIOINGIZA MKWANJA MREFU MWAKA 2021

JAY Z, KANYE WEST & DIDDY WATAJWA KAMA MARAPA WALIOINGIZA MKWANJA MREFU MWAKA 2021

Orodha ya wasanii wa Hip Hop waliotengeneza pesa nyingi zaidi mwaka wa 2021 imetoka na jina la Jay-Z lipo namba 1.

Jay Z ametajwa kuingiza kiasi cha shilling billion 51.2 za Kenya  ambazo zimetokana na pato la baada ya kuuza hisa zake nyingi za mtandao wa TIDAL kwa kampuni ya Square Ink, kwa takriban shilling billion kiasi cha shilling billion 34.4 za Kenya.

Lakini pia Jay Z alikunja mkwanja mrefu mwaka jana baada ya kampuni ya LVMH kununua nusu ya hisa za Kinywaji chake, cha Armand de Brinac.

Kwa upande wa Kanye west ambaye amekamata nafasi ya pili kwa shilling billion 28.5 za Kenya, pato lake kubwa limeendelea kuingia kupitia bidhaa za Yeezy.

Wasanii wengine waliongiza pesa nyingi mwaka wa 2022 ni pamoja na Diddy ambaye alikamata nafasi ya tatu kwa shilling billion 8.5 akifuatwa na drake aliyeingiza kiasi cha shilling billion 5.7 huku tano bora ikifungwa na mtu mzima wiz khalifa ambaye aliingiza kiasi cha shilllingi billion 5.1 za Kenya.

HIP-HOP’S TOP EARNERS 2021

 1. JAY-Z – $470 million
 2. Kanye West – $250 million
 3. Diddy – $75 million
 4. Drake – $50 million
 5. Wiz Khalifa – $45 million
 6. Travis Scott – $38 million
 7. DJ Khaled – $35 million
 8. Eminem – $28 million
 9. J. Cole – $27 million
 10. Birdman – $25 million
 11. Doja Cat – $25 million
 12. Tech N9ne – $25 million

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke