Rapa mkongwe kutoka Marekani Jay-Z ameamua kumfikisha mahakamani aliyekuwa mpiga picha wake kwa madai ya kutumia picha zake Kibiashara bila idhini yake.
Baada ya kushindwa kufikia makubaliano nje ya mahakama, sasa shtaka hilo limetajwa kuwa litaanza kusikilizwa Julai 22 mwaka huu.
Mwaka jana Jay-Z alifungua mashtaka akidai kwamba mpiga picha huyo aitwaye Jonathan Mannion ambaye alihusika kupiga picha zilizotumika kwenye album cover ya ‘Reasonable Doubt’ alichukua picha zilizobaki na kuziuza kwenye tovuti yake bila idhini.