You are currently viewing Jay-Z na Jonathan Mannion wamaliza tofauti zao nje ya mahakama

Jay-Z na Jonathan Mannion wamaliza tofauti zao nje ya mahakama

Jay-Z ameafikiana na Jonathan Mannion kwenye shtaka ambalo Rapa huyo mkongwe na Mfanyabiashara alimshtaki mpiga picha huyo ambaye alikuwa nyuma ya cover za Album kama ‘Reasonable Doubt, ‘Hard Knock Life’ na The Blueprint.

Hov alimshtaki Mannion na Kampuni yake mwezi June 2021 kwa madai ya mpiga picha huyo kunufaika kupitia Jina lake kwa kuuza picha zake kwenye tovuti pasina ridhaa. Malalamiko hayo yalidai Mannion amekuwa akitengeneza Maelfu ya Dola za Kimarekani.

Baada ya Jay-Z na Roc Nation kumpiga marufuku, Mannion alidaiwa kutaka kitita kirefu cha pesa. Shtaka hilo lilitajwa kuanza kuunguruma Mahakamani mwezi March mwaka huu, lakini Jay-Z na Jonathan Mannion wanaonekana kuwa tayari wameyamaliza nje ya Mahakama hivyo shtaka hilo halitofika tena Mahakamani.

Kwa mujibu wa nyaraka za Mahakama zilizodakwa na mtandao wa AllHipHop, Jay-Z na Jonathan Mannion wamemuomba Jaji kuiondoa kesi hiyo Mahakamani wakieleza kwamba wamekubaliana kumalizana. Mahakama imewataka kuwasilisha hati za makubaliano yao hadi Februari 17 mwaka huu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke