You are currently viewing JENNIFER LOPEZ AFUNGUKA JUU YA PETE GHALI ALIYOVISHWA NA BEN AFFLECK

JENNIFER LOPEZ AFUNGUKA JUU YA PETE GHALI ALIYOVISHWA NA BEN AFFLECK

Mwanamuziki kutoka marekani Jennifer Lopez amefunguka nyuma ya pazia kuhusu tukio la kuvalishwa Pete ya uchumba na Ben Affleck.

Katika mahojiano na chombo kimoja cha Habari, Mwanamama huyo amesema haikuwa kama alivyozoea kwani Ben alimkuta mtupu akiwa anaoga kwenye ‘Bubble Bath’

Pete ya Jennifer Lopez inatajwa kuwa na thamani ya ($10 million) ikiwa ni ghali zaidi kuwahi kuvalishwa na wanaume aliowahi kuwa nao kwenye mahusiano.

J-Lo alianza mahusiano na Ben Affleck ambaye ni nyota wa filamu Marekani mwaka 2002 baada ya kutalikiana na mume wake wa pili Cris Judd, waliingia kwenye uchumba November 2002 na kupanga kuoana September 2003 lakini ndoa hiyo iliahirishwa kutokana na kuandamwa na vyombo vya habari. Uchumba wao ulivunjika rasmi January 2004.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke