You are currently viewing JOE BOY AWATOLEA UVIVU WAANDAJI WA AFRO JAM FESTIVAL

JOE BOY AWATOLEA UVIVU WAANDAJI WA AFRO JAM FESTIVAL

Nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria Joeboy amewatolea uvivu waandaji wa tamasha lla Afro Jam mara baada ya tamasha hilo lilofanyika Disemba 11 Jiji Nairobi kukumbwa na changamoto lukuki.

Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa instagram Joe Boy ametoa ya moyoni kwa kusema kwamba aliumizwa na kitendo cha ala za muziki kukwama akiwa jukwaani kwenye tamasha hilo kutokana na ubovu wa sauti jambo ambalo anadai lilimlazimu kuondoka jukwaani kabla ya muda wake kujakamilika.

Hitmaker huyo wa “Alcohol” amewataka waandaji wa matamasha ya muziki kuwekeza kwenye vyombo vya sauti iwapo wanataka wasanii watumbuize kwenye matamasha yao kwa manufaa ya mashabiki na wasanii kwa ujumla.

Hata hivyo amewashukuru wakenya kwa upendo waliyomuonyesha kwenye tamasha la Afro Jam licha ya tamasha hilo kugubikwa na changamoto kibao.

Ikumbukwe Joe Boy alikuwa amesindikizwa na wasanii kama Khaligraph Jones, Trio Mio,Nikita Kering ila mpaka sasa haajatoa tamko lolote kuhusu tamasha la Afro Jam.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke