Rappa na Mtangazaji kutoka nchini Marekani Joe Budden hajaona sababu yoyote ya kuikalia kimya kauli ya rappa Jay Z kuto toza kiasi chochote cha pesa katika ngoma anazo shirikishwa.
Akiwa kwenye Episode mpya ya Flip Da Script podcast, Budden amesema Jay Z aliwahi kumtoza kiasi cha $250k ili kumpata kwenye remix ya ngoma yake ya “Pump It Up”
Utakumbuka hivi katibuni Jigga alifanya mahojiano na Mchekeshaji Kevin Hart kupitia podcast ya “Hart to Heart” ambapo alifunguka kuto toza kiasi chochote cha pesa katika nyimbo anazoshirikishwa.