Msanii wa Hip Hop Bongo kutoka kundi la Weusi, Joh Makini amesema mashabiki wanaoulizia ilipoishia kolabo yake na mwimbaji wa Nigeria, Simi, majibu yake watayapata kwenye albamu yake mpya.
Joh Makini amesema si kolabo na Simi tu, bali hata alizofanya na wasanii wengine kama Fallz, Y Cee na Cassper Nyovest na kuzitangaza kwa mashabiki wake.
“Hizo zote ni project zangu, wakati albamu yangu inatoka watapata maelezo yote,” amesema Joh Makini.
Miaka ya hivi karibuni Simi amevuma sana barani Afrika mara baada kuachia nyimbo zake kama Gone For Good, Love Don’t Care, Jericho, Joromi na Duduke.
Ikumbukwe tayari Joh Makini amefanikiwa kufanya kazi na wasanii wa Nigeria kama Davido aliyemshirikisha katika wimbo ‘Kata Leta’ na Chidinma aliyekutana naye kwenye msimu wa nne wa Coke Studio Afrika mwaka 2016 na baadaye wakaachia wimbo uitwao Perfect Comb.