Msanii wa Hip Hop Bongo kutoka kundi la Weusi, Joh Makini amekanusha vikali madai ya Sallam SK kuhusu kolabo yake na Rapa wa Afrika Kusini, AKA.
Katika show ya The Joint ya Dizzim TV, Sallam SK alidai kuwa yeye ndiye aliyeunganisha kolabo ya Joh Makini na AKA (Don’t Bother) bila malipo yoyote.
Joh Makini kupitia mtandao wa Twitter ameonyeshwa kushangazwa na kauli hiyo, huku akimtaja mtu anayetambulika kama ‘Mwarabu’ kufanya mpango wa kukwamisha kolabo hiyo.
“Aeleze aliunganisha vipi, kwa mazingira niliyofanya collabo na AKA nitawashukuru sana Nikki wa Pili na G Nako lakini waliomleta walikuwa hawataki itokee” amesema.
“Yeye sio chanzo cha hiyo collabo. Mwarabu alipambana sana kukwamisha hii basi tu Mwenyenzi Mungu huwa hajawahi kushindwa,” amesema Joh Makini.
Utakumbuka ngoma ya Don’t Bother ambayo Joh Makini kamshirikisha AKA ilitoka Novemba mwaka wa 2015 chini ya Producer, Nahreel, video yake ilifanyika Afrika Kusini, Director wake ni Justin Compas kutoka Gorilla Films.