You are currently viewing JOSE CHAMELEONE AFUNGUKA SABABU ZA KUTOACHA MUZIKI

JOSE CHAMELEONE AFUNGUKA SABABU ZA KUTOACHA MUZIKI

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Jose Chameleone amefunguka sababu za kutostaafu kwenye muziki licha ya kufanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 20.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Chameleone amesema muziki upo ndani damu yake na hivyo haoni kabisa akiacha kuimba.

Bosi huyo wa lebo ya Leone Island amesema hafanyi tena muziki kwa shinikizo za kupata pesa kama miaka ya hapo nyuma kwa sababu ana mali nyingi.

“Sasa natoa muziki ninapojisikia kwa sababu sifanyi kwa ajili ya kujinufaisha kifedha. Tayari nina mali,” alisema katika mahojiano na runinga moja nchini Uganda.

Ikumbukwe Jose Chameleone amejipatia mali nyingi kupitia muziki wake na anaendelea pia kuwekeza kwenye biashara mbali mbali.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Forever” ana mjengo wa kifahari huko Seguku nchini Uganda lakini pia inasemekana kuwa ana nyumba mbili nchini Marekani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke