You are currently viewing JOSE CHAMELEONE AKIRI BIFU LAKE NA WASANII GOODLYFE CREW LILIMSAIDI KUKUA KIMUZIKI

JOSE CHAMELEONE AKIRI BIFU LAKE NA WASANII GOODLYFE CREW LILIMSAIDI KUKUA KIMUZIKI

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Jose Chameleone amekiri kuwa bifu yake na wasanii wa Goodlyfe Crew Mozey Radio na  Weasel Manizo lilimsaidia kukua kimuziki.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Chameleone amesema kuwa bifu zinasaidia kukuza muziki kwani kipindi cha nyuma alipokuwa anajibu diss tracks za wasanii hao kwa kuachia ngoma alizungumziwa sana kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.

Lakini pia ugomvi wake  na wasanii wa Goodlife Entertainmet uliwatengenezea wasanii hao brand yao ya muziki.

Utakumbuka mwaka wa 2005 wasanii wa Goodlyf Crew walikuwa kwenye ugomvi mkali na chameleone jambo lilowafanya kuachia nyimbo za kumshambulia chameleone wakimtaja kama shetani lakini pia msanii wa mashinani.

Hata hivyo walikuja baadae wakaweka kando tofauti zao kwa faidi ya wapenzi wa muziki mzuri nchini Uganda ambao waliingia kati na kuwataka wasanii hao waache ishu ya kuendekeza chuki na badala yake washirikiane kwenye shughuli zao za kimuziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke