You are currently viewing JOSE CHAMELEONE AKIRI KUSHINDWA NA MASUALA YA SIASA

JOSE CHAMELEONE AKIRI KUSHINDWA NA MASUALA YA SIASA

Msanii nguli kutoka Uganda Jose Chameleone amekiri kutokuwa na bahati kwenye masuala ya siasa ikiwa ni mwaka mmoja tangu apoteze kiti cha umeya wa jiji la kampala kwa mpinzani wake Erias Lukwago katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021.

Akizungumza kwenye moja ya show huko Mukono Chameleone amesema amekubali hatma yake kwenye siasa huku akidai bado ana ari ya kutaka kujua kiini cha watu kutompigia kura kwenye wadhfa wa umeya licha ya kuwa na mashabiki wengi katika muziki wake.

Bosi huyo wa Leone amethibitisha kutorudi tena kwenye masuala ya siasa na badala yake ataelekeza nguvu zake kufanya muziki ambao umekuwa ukimuingizia kipato kwa miaka nyingi.

Hata hivyo amedokeza ujio wa show kubwa kati yake  na bebe  cool baada ya show yao iitwayo The Battle of champions iliyokuwa ikiwashindanisha huko Mukono nchini Uganda kupata mapokezi mazuri kutoka kwa mashabiki zao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke