You are currently viewing JOSE CHAMELEONE AMFUTA KAZI MENEJA WAKE BIJOU FORTUNATE KISA UZEMBE KAZINI

JOSE CHAMELEONE AMFUTA KAZI MENEJA WAKE BIJOU FORTUNATE KISA UZEMBE KAZINI

Bosi wa lebo ya leone island Jose Chameleone amemfuta kazi meneja wake Bijou Fortunate.

Inadaiwa kuwa Bijou ameshindwa kumleta Chameleone dili kubwa za kimataifa kitu ambacho kimemfanya msanii huyo kutoridhika na utenda kazi wake.

Hata hivyo duru za kuaminika zinasema kuwa chameleone anafadhalisha kufanya kazi na meneja wake zamani Robert Mutiima ambaye kipindi cha nyuma alimleta dili nyingi zilizomuingizia kipato.

Ingawa hakuna tamko rasmi kutoka kwa Chameleone ila chanzo cha karibu na msanii huyo kinasema Robert Mutiima ameamuriwa kuchukua wadhfa wa umeneja wa kazi za Chameleone.

Bijou alitambulishwa kama meneja wa Chameleone mwaka wa 2020 ila wengi walitilia shaka uwezo wake wa kusimamia kazi za msanii huyo ambapo walienda mbali zaidi na kusema kuwa mrembo huyo hawezi kaa mwezi mmoja lakini aliwashangaza wakosoaji wake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke