You are currently viewing Jose Chameleone atakiwa kuzindua kampuni yake ya simu

Jose Chameleone atakiwa kuzindua kampuni yake ya simu

Msanii mkongwe kutoka nchini Uganda Jose Chameleone ameshauriwa kutekeleza mpango wake wa kuanzisha mradi wake kufungua kampuni ya simu iitwayo Chameleone Phones.

Wito huo umetolewa na mwanahabari Douglas Lwaga ambaye amehoji kuwa Chameleone alipoteza fursa kubwa ya kuingiza pesa nyingi kupitia mpango wake wa kuzindua kampuni ya simu.

Hata hivyo amesema msanii huyo mkongwe ana nafasi nyingine ya kufaulu kibiashara kupitia wazo lake hilo kwa kuwa ana bado ana ushawishi kwenye tasnia ya muziki Afrika mashariki na barani Afrika kwa ujumla.

“Jose Chameleone missed out on a huge opportunity of launching the Chameleone Phone. This could have brought him lots of cash. I think he can still go for it,” Alisema kwenye kipindi cha runinga cha After 5 show.

Utakumbuka zaidi mwongo mmoja uliopita Jose Chameleone alikuwa na mpango wa kuzindua kampuni yake ya simu iitwayo Chameleone Phone lakini hakufanikiwa kutekeleza mpango wake huo kwa sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke