You are currently viewing JOSE CHAMELEONE MBIONI KUACHIA COLLABO YAKE NA KOFFI OLOMIDE

JOSE CHAMELEONE MBIONI KUACHIA COLLABO YAKE NA KOFFI OLOMIDE

Bosi wa lebo ya muziki ya Leone Island Jose Chameleone amekuwa jamhuri ya demokrasi ya kongo kwa kipindi cha wiki moja sasa.

Goods ni kuwa Chameleone ameonekana kuingia studio na nguli wa muziki barani afrika Koffi Olomide jambo linalotafsiri kuwa huenda kukawa na kazi ya pamoja baina ya wawili hao hivi karibuni.

Duru za kuaminika zinasema wawili hao walitumbuiza pamoja mapema wiki hii huko Kinshasa ambapo walipiga shoo ya kufa mtu ambayo iliwavutia watu wengi zaidi.

Jose chameleone anajiunga na wasanii wa afrika mashariki Diamond platinumz na Nandy ambao tayari wamefanya kazi na Koffi olomide ambaye ni moja kati ya wasanii wakubwa jamhuri ya demokrasia ya congo

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke