Bosi wa lebo ya muziki ya Leone Island msanii Jose Chameleone ameweka wazi kwamba hana mpango tena wa kuingia kwenye siasa.
Chameleone amesema siasa inataka pesa nyingi sana na kwa mantiki hiyo itakuwa vigumu kwake kuwania wadhfa wowote wa kisiasa.
Hata hivyo amesisitiza kwamba licha ya watu kutompigia kura kwa wingi kwenye uchaguzi mkuu uliopita nchini Uganda, anaamini hana vigezo vya kuwa kiongozi na ndio maana wananchi walimchagua mpinzani wake.
Ikumbukwe Jose Chameolene alipoteza kwenye uchaguzi wa umeya wa Jiji la Kampala mapema mwaka huu na mpinzani wake Erias Lukwago.