Msanii nyota nchini Jovial amedokeza ujio wa EP yake mpya ambayo itaiachia ndani ya mwaka huu wa 2022.
Katika mahojiano na Mungai Eve, Jovial amesema kwa sasa yupo chimbo anaanda EP mpya ambayo amedai kuwa itakuwa na ladha ya kitofauti sana kutokana na wasanii atakaowashirikisha kwenye kazi hiyo.
Licha ya kutoweka wazi idadi ya ngoma na tarehe ambayo Ep yake hiyo itaingia sokoni, Jovial amewataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kupokea ujio wake mpya ambao utakuwa wa moto wa kuotea mbali sana.
Utakuwa mapema mwaka wa 2020 Jovial aliahidi mashabiki zake kwamba ataachia EP mpya lakini hakufanikiwa kufanya hivyo kutokana msala wa Corona jambo ambalo lilimpelekea kusitisha mchakato mzima wa kutayarisha project hiyo.