Female singer kutoka Kenya Jovial amekanusha madai yanayotembea mtandaoni kuwa anatoka kimapenzi na DJ maarufu nchini Sami Flinch.
Katika kikao cha maswali na mashabiki zake kwenye mtandao wa Instagram Jovial amesema madai hayo hayana msingi wowote huku akisema ukaribu wao ulitokana na shughuli za kikazi ambazo walikuwa nayo kipindi cha nyuma.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Pita Nawe” amesema kwa ngazi aliyofika kwa sasa anahitaji zaidi pesa kuliko mpenzi huku akithibitisha kuwa hayupo kwenye mahusiano.
Hata hivyo amesema skendo za mtandaoni hazina nafasi kwa sasa katika maisha yake kwani anahitaji kuacha mashabiki wake wapate wanachostahili kupitia muziki wake.