You are currently viewing Jovial akanusha uvumi wa kutoka kimapenzi na Willy Paul

Jovial akanusha uvumi wa kutoka kimapenzi na Willy Paul

Msanii wa kikw kutoka Kenya Jovial  kwa mara ya kwanza amevunja kimya chake kuhusu uvumi wa kutoka kimapenzi na msanii mwenzake Willy Paul.

Akimjibu shabiki kupitia ukurasa wake wa Facebook, Jovial ameweka wazi kuwa Pozee sio mpenzi wake kama watu wanavyodai mitandaoni huku akisisitiza kuwa uhusiano wake na bosi huyo wa saldido ulikuwa wa kikazi tu na si vinginesvyo.

“Je, Pozee ni mpenzi wako wa dhati?” Shabiki mmoja aliuliza. Jovial akamjibu “Itoshe! Pozee si mpenzi wangu! Ni rafiki tu, ilikuwa biashara ambapo sote tulipata faida! Kwa sasa tumerudi kwa maisha yetu ya kawaida,.

Hitmaker huyo wa Mi Amor amesema ameamua kufichua hayo kwa kuwa ameshindwa kuvumilia maswali ya walimwengu wanaolazimisha uhusiano wake na Willy Paul wakati hakuna kitu inaendelea kati yao.

“Nimekabwa na maswali yenu! Mungu anisaidie kwa yatakayofuata! Aiii! Mayooo!” ameandika Jovial.

Utakumbuka wawili hao walihisiwa kutoka kimapenzi walipojiachia kimahaba Zaidi miezi kadhaa iliyopita wakati walikuwa watangaza wimbo wao wa pamoja uitwao “Lalala”

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke