Msanii nyota nchini Jovial amechukizwa na kitendo cha mwanaume mmoja kumkosesha amani nyakati za usiku kwa kumtaka kimapenzi.
Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram amesema mwanaume huyo ambaye kipindi cha nyuma aliagiza chakula kutoka kwake, amegeuka kuwa kero kwake kwa kumpigia simu kila mara jambo ambalo amedai limemkosesha usingizi.
Hitmaker huyo wa “Mi Amor” ameenda mbali na kusema licha ya kuwa anashukuru kwamba jamaa huyo ni shabiki yake kimuziki, hatowavumilia watu sampuli hiyo ikizingatiwa kuwa anapenda kuishi maisha yake ya faraghani bila muingilio wa mtu yeyote.
Hata hivyo ameutaka uongozi wake kuhamkikishia usalama kwavkubadilisha laini yake ya simu kwani amekuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa watu wasiojulikana.