Female singer kutoka Kenya Jovial amefunguka na kudai kwamba hatokuja kumsamehe mwanaume yeyote anayemtelekeza mwanamke akiwa mja mzito kwani ujauzito ni kama ugonjwa.
Kupitia Whatsapp Story yake Hitmaker huyo wa ngoma ya “Pita Nawe” ameandika ujumbe unaosomeka “Siwezi msamehe mwanaume anayemtelekeza mwanamke mjamzito mimba ni kama ungojwa asikuambie mtu unahitaji upendo wote mshukuru Mungu “
Kauli yake Jovial imekuja mara baada ya chapisho la mwanamke mmoja kusambaa mtandaoni akieleeza namna alivyotelekezwa na mpenzi wake akiwa mjamzito na baada ya kupata usaidizi kutoka kwa mwanaume mwingine,mpenzi wake wa zamani sasa anataka warudiane tena ikiwa ni miaka mitano tangu amkimbie.