You are currently viewing JOVIAL ATHIBITISHA KUKAMILIKA KWA EP YAKE MPYA

JOVIAL ATHIBITISHA KUKAMILIKA KWA EP YAKE MPYA

Staa wa muziki nchini Jovial kwa mara ya kwanza ametusanua kuhusu maendeleo ya EP yake mpya ambayo itaingia sokoni ndani ya mwaka huu.

Kupitia Inststory yake kwenye mtandao wa Instagram yake Jovial amethibitisha kukamilika kwa EP hiyo ambayo amedai kuwa ni ya kitofauti kwa sababu imebeba nyimbo ambazo ameimba kwenye mitindo mbali mbali.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Jeraha” amesema kutayarisha EP hiyo haijakuwa jambo rahisi kwake kwa kuwa amepitia changamoto nyingi ambazo amedai nusra zimekatishe tamaa ila kwa sasa anamshukuru kwa kumsimamia hadi kukamilika kwa EP yake mpya.

Mrembo huyo amewashukuru maprodyuza waliohusika kwenye uandaji wa EP yake kwa kusema bado anafanya marekebisho kwa baadhi ya nyimbo kabla ya kuachia rasmi ep yake.

Hata hivyo hajatuambia jina ya EP, idadi ya ngoma itakayopatikana kwenye ep hiyo na tarehe rasmi ambayo ataachia kazi hiyo kwa mashabiki zake ila ni jambo la kusubiriwa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke