You are currently viewing JOVIAL AWACHANA WANAOKOSOA KWA KUCHEZA KIMAHABA NA RASHID ABDALLA

JOVIAL AWACHANA WANAOKOSOA KWA KUCHEZA KIMAHABA NA RASHID ABDALLA

Msanii wa kike nchini Jovial amewatolea uvivu wanaomkosoa kwa kucheza kimahaba na Rashid Abdalla ambaye ni mume wa mwanahabari maarufu nchini Lulu Hassana kwenye birthday yake juzi kati.

Kupitia instastory kwenye mtandao wa Instagram Jovial amesema ameshangazwa na hatua ya wanawake kumshambulia mitandaoni kwa kitendo cha kucheza kimahaba na rashid abdalla huku akisema jambo hilo inaonyesha ni jinsi gani wanawake wanamuonea wivu mitandaoni wana matatizo mengi kwenye ndoa zao.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mi Amor” amesema hakuwa na nia ya kumnyanganya lulu hassan mume wake kama wengi wanavyodai kwenye mitandao ya kijamii kwani alikuwa anatoa tu burudani kwa watu waliokuwa wamehudhuria hafla ya kusherekea kumbukizi ya kuzaliwa kwa mwanahabari huyo.

Hata hivyo amewataka wanawake wanaomkosoa kutatua changamoto zinazowakumba kwenye ndoa zao badala ya kumzushia madai ambayo hayana msingi wote mitandaoni akiwa kwenye shughuli inayomuingizia riziki.

Kauli Jovial imekuja mara kupata ukosoaji mkubwa kutoka kwa walimwengu kutokana na video inayosambaa mtandaoni ikimuonyesha akicheza kimahaba na Rashid Abdalla kwenye  birthday yake kitendo kilichomfanya Lulu hassan aingilie kati kumzuia msanii huyo asiendelee kucheza na mume wake kimahaba zaidi kwenye performance yake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke