You are currently viewing JOVIAL AWAJIBU WANAOMTAKA KUTOA MSAADA KWA JAMII

JOVIAL AWAJIBU WANAOMTAKA KUTOA MSAADA KWA JAMII

Mkali wa sauti na maandishi ya muziki, Jovial, amewatolea uvivu baadhi ya watu wanaomshinikiza kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji kwenye jamii.

Kupitia instastory yake, Hitmaker huyo wa ‘Mi Amor’ amefichua kwamba amekuwa akipokea jumbe nyingi (DM) kutoka kwa mashabiki, wakihoji kwa nini hawasaidii watu wenye uhitaji na wasanii chipukizi wakati ana mafanikio makubwa kwenye muziki.

Akipuzilia mbali pendekezo hilo, Jovial amesema kumsaini msanii kwenye lebo ya muziki ni biashara yenye athari za kisheria huku akisisitiza kuwa suala la kutoa misaada kwa jamii sio la kutangazwa au kuonyeshwa kwenye mitandao ya kijamii bali ni siri kati yake na mwenyezi Mungu.

“The emotional blackmail on DM, about giving back to the society, specifically signing new artistes. Well giving back is a secret between me and my God, I do not do the social media parade,” Jovial alisema.

“And please let us be exposed, signing an artist is not giving back to the community, it is business. I sign you, and you bring me money, You screw up, and I take you to court,” aliongeza.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke