Kumbe mrembo Julia Fox hakuwa na mapenzi kabisa kwa rapa Kanye West, ni vile tu alipenda pesa zake.
Kwenye video ambayo aliiweka TikTok hivi karibuni, mrembo huyo ambaye alikuwa penzini na YE tangu Disemba 2021 hadi Februari 2022 amekiri kuwachukia matajiri ambapo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba anatamani hata wasiwepo duniani.
“Pesa zinazotoka kwa mabilionea zinatakiwa kurudi kwenye Jamii ambayo iliwafanya wawe matajiri. Huu ndio mtazamo wangu kuhusu mabilionea, hawatakiwi kuwepo kabisa kwenye Jamii yetu. Ndio maana nimekuwa nikiwatumia, sijawahi kupenda yeyote kati yenu ninyi watu.” Alisema