You are currently viewing JULIANI AKIRI KUPOTEZA DILI NONO KISA MKE WAKE LILIAN NG’ANG’A

JULIANI AKIRI KUPOTEZA DILI NONO KISA MKE WAKE LILIAN NG’ANG’A

Rapa kutoka Kenya Juliani amefichua kuwa alipoteza dili mbili kubwa baada ya kuingia kwenye mahusiano ya kimpenzi na Lilian Ng’ang’a mwaka 2021.

Akizungumza na Kalondu Musyimi, Juliani amesema makampuni yalioyolenga kufanya nae kazi kipindi hicho yaliingiwa na hofu kutokana na namna watu walivyokuwa wakimshambulia mtandaoni.

Juliani hata hivyo ametoa changamoto kwa vyombo vya habari kuwakuza wasanii wa Kenya badala ya kuwapigia simu pale wanapofuatilia habari za udaku.

Mapema wiki hii Juliani aliingia kwenye vichwa vya habari za burudani baada ya baadhi ya watumiaji mitandao ya kijamii kumfananisha na aliyekuwa gavana wa Machakos Alfred Mutua ambaye awali alikuwa akichumbiana na Lilian Ng’ang’a.

Walimwengu walienda mbali zaidi na kuhoji ni kwa nini Lilian aliamua kumwacha Mutua mwenye utajiri mkubwa na kuishia kuingia kwenye mahusiano na Juliani ambaye walidai anasuasua kiuchumi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke