Rapa Juliani ametangaza ujio wa tamasha lake liitwalo Nairobi Startup week ambayo ni mahususi kwa ajili ya wafanyibiashara wadogo na wale wa kadri.
Juliani amethibitisha taarifa hiyo kwenye ukurasa wake wa instagram kwa kusema kuwa tamasha hilo la siku tano litaanza rasmi Julai 10 hadi julai 15 huko Waterfront mall jijini Nairobi ambapo itajumuisha maonesho ya bidhaa na burudani kutoka kwa wasanii mbali mbali.
Rapa huyo amesema nia yake kuja na tamasha hilo ni kwa ajili ya kuonesha na kusherekea umuhimu wa jamii ya wafanyibiashara wadogo na wale wa kadri katika ujenzi wa taifa.