Hatimaye mwanamuziki Juliani amefunguka kuhusu kinachoendelea mitandaoni kumuhusu mke wake Lilian Ng’ang’a.
Kupitia ukurasa wake wa twitter ameamua kutoa maelezo kuhusu hali yake ya uchumi kwa kuwakejeli wanaomsema vibaya mtandaoni.
Rapa huyo ameandika ujumbe anaosema kwamba amefulia kiuchumi ambapo ameenda mbali zaidi na kuwaomba wakenya msaada wa kifedha kupitia paybill ili aweze kumnunulia mtoto wake pampers.
“Wase! Nikubaya niko BROKE! mtoi anahitaji pampers. Please send mpesa. Paybill: Business number – 784577 Account- Juliani Chochote unaeza itasaidia. Yours truly, Struggling rapper/entrepreneur”, Ameandika Juliani.
Ujumbe huo umezua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii wengi wakihoji kuwa huenda amewajibu kimtindo wanaodai kuwa anaishi maisha ya uchochole huku wengine wakimshushia kila aina matusi kwa hatua ya kukimbia na mke wa Alfred Mutua.