Msanii mkongwe wa Bongofleva, Juma Nature amesema anajiandaa kuachia albamu yake mpya ambayo imekamilika.
Nature amesema anachokifanya kwa sasa ni kutayarisha video kadhaa za nyimbo zinazopatikana kwenye albamu hiyo kabla ya kuingia sokoni hivi karibuni.
Hata hivyo Sir Nature hajatuambia jina la album, idadi nyimbo na wasanii aliyowashirikisha kwenye album yake hiyo ila ni jambo la kusubiriwa.
Utakumbuka Juma Nature ana historia ya kuwa msanii wa kwanza Bongo kuujaza ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam katika uzinduzi wa albamu yake iitwayo Ugali.
Wasanii wengine tanzania ambao tayari wametangaza kukamilika kwa albamu zao ni pamoja na Diamond Platnumz, Harmonize, Marioo, Young Lunya, Lava Lava, Tommy Flavour, Maua Sama, Ommy Dimpoz na wengine wengi.