Jumba la Rapa Drake lililopo mjini Los Angeles nchini Marekani limevamiwa na mtu mmoja ambaye alivunja na kufanikiwa kuingia ndani. Baada ya muda mfupi, polisi waliwasili kufuatia simu iliyopigwa na walinzi wa nyumba wakidai kumuona mtu mmoja akitokomea akiwa amebeba kitu.
Baada ya msako wa nje na maeneo ya Jirani, alipatikana mtu mmoja ambaye alihisiwa kuwa ndiye mwizi. Polisi walimtia mbaroni na kumkuta akiwa amebeba vitu ambavyo vinaaminika alivitoa nyumbani kwa Drizzy ikiwemo picha za michoro. Tovuti ya TMZ inaripoti, Drake hakuwepo nyumbani wakati tukio linatokea.