You are currently viewing JUSTIN BIEBER AFUTA KESI DHIDI YA WANAWAKE WAWILI WALIODAI KUWA AMEWABAKA

JUSTIN BIEBER AFUTA KESI DHIDI YA WANAWAKE WAWILI WALIODAI KUWA AMEWABAKA

Staa wa muziki wa pop Duniani Justin Bieber amefuta shauri la Kashfa (Defamation) dhidi ya wanawake wawili ambao walidai kunyanyaswa kijinsia na mkali huyo toka nchini Canada.

Bieber alifungua shauri hilo akidai zaidi ya Shillingi billion 2.3 za Kenya baada ya kupangua madai yote mawili.

Mwanamke wa kwanza aliyefahamika kwa jina ‘Danielle’ alidai kubakwa na Justin Bieber mwaka 2014 kwenye chumba kimoja cha hoteli mjini Texas.

Hata hivyo Justin Bieber alikanusha taarifa kwa kuachia ukweli kwamba siku hiyo tajwa pamoja na muda, hakuwepo Texas bali alikuwa na aliyekuwa mpenzi wake, Selena Gomez.

Mwanamke wa pili aitwaye Khadidja Djibrine pia alidai kunyanyaswa kingono na mwimbaji huyo mwaka 2015 lakini Bieber aliibuka tena na kukanusha.

Aidha alitumia mtandao wa Twitter kukazia hilo kwa kusema kuna vitu vya kuvumilia lakini sio tuhuma za unyanyasaji wa Kingono.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke