Justin Bieber ametangaza kuahirisha ziara yake ya “Justice World Tour” kufuatia matatizo ya Kiafya. Ziara hiyo iliyoanza toka Machi mwaka huu na sasa ikiwa imebakiza show 70 hadi mwezi Machi 2023, sasa show hizo zimeahirishwa.
Bieber amesema sababu ya kuahirisha maonesho hayo ni kuimarisha afya yake. Baada ya kumaliza onesho lake nchini Brazil, Bieber alisema “Niliposhuka tu Jukwaani, uchovu mzito ulinishika na nikagundua kwamba nahitaji kuiweka afya yangu kama kipaumbele.” alikaririwa JB na kumalizia kwa kusema anabidi achukue mapumziko kwa muda.
Mwezi Juni mwaka huu Justin Bieber alimamisha muendelezo wa ziara hiyo kufuatia kukutwa na tatizo la Ramsay Hunt syndrome, ambalo lilipelekea kupoozesha kwa muda upande mmoja wa uso wake. Baada ya mwezi mmoja ziara hiyo ilitangazwa kurejea tena.