Nyota wa muziki wa pop duniani Justin Bieber ametangaza kuja na ziara yake ya ‘Justice World Tour’ mjini Cape Town Afrika Kusini, September 28 mwaka wa 2022.
Siku mbili zilizopita Justin Bieber alianika mkeka wa mataifa na miji ambayo ziara yake hiyo itapita kwa takribani mwaka mzima hadi Machi mwaka wa 2023.
Afrika Kusini ndio taifa pekee barani Afrika ambalo Justin Bieber atapita na ziara hiyo ilipangwa kuanza Mei 14 mwaka wa 2020 lakini iliahirishwa mara mbili kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19