You are currently viewing JUSTINA SYOKAU ATAKA SERIKALI YA WILLIAM RUTO KUWASAIDIA WASANII

JUSTINA SYOKAU ATAKA SERIKALI YA WILLIAM RUTO KUWASAIDIA WASANII

Mwimbaji wa nyimbo za injili Justina Syokau ametoa wito kwa serikali ya Rais William Ruto kutengeneza mazuri kwa wasanii waweze kuingiza kipato kupitia muziki wao.

Akizungumza na Nicholas Kioko, Syokau amesema kwa kipindi kirefu wasanii wamekuwa wakisuasua kiuchumi kutokana na ukosefu mifumo rafiki ya kufanya muziki kibiashara zaidi.

Hitmaker huyo wa “2020” ametaka serikali kupunguza kodi kwenye baadhi ya huduma ili wasanii wafaidi na sanaa yao kwa kuwa wengi wamekwama kiuchumi licha ya kutumia pesa nyingi kuwekeza kwenye muziki.

Sanjari na hilo amekanusha kuiba mashairi ya wimbo wa “Maombi” wake msanii Nadia Mukami na kutumia kwenye wimbo wake mpya ambao aliuimba mahususi kwa ajili ya rais wa tano wa Kenya William Ruto.

Mwanamama huyo amesema madai hayo hayana ukweli wowote bali yaliibuliwa na baadhi ya watu wanamuonea wivu kwa mafanikio aliyoyapata kwenye muziki wake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke