Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Kenya Justina Syokau amechukua headlines za mitandao ya kijamii baada ya kushare picha inayomuonesha akiwa na muonekano mpya huku akidai kufanya upasuaji wa kuongeza ukubwa wa makalio yake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Syokau ameandika “Hatimaye nimefanikisha lengo langu la kupata makalio makubwa. Napenda muonekano wa mwili wangu mpya,”
Haijulikani kama alifanya upasuaji wa kuongeza makalio ila walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamehoji amehariri picha ili kuonekana ana makalio makubwa.
Ikumbukwe miezi kadhaa iliyopita wakati Vera Sidika alipowahadaa watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwa amefanya upasuaji wa kupunguza makalio kutokana na matatizo ya kiafya, Syokau katika mahojiano na podcast ya mtangazaji Mwende Macharia alisema kuwa hata yeye alikuwa na wazo la kufanya upasuaji ili kuongeza makalio yake.
Mwanamama huyo alisema kuwa hatua yay eye kuongeza makalio sio tu kuwavutia wanaume bali ilikuwa njia moja ya kutumia muonekano wa mwili wake kusambaza neon la Mungu.