Huenda msanii nyimbo za injili Justina Syokau akaenda kufanya ‘Surgery’ kama baadhi ya mastaa wengine walivyofanya ili kuboresha muonekano wake.
Hitmaker huyo wa 2020 amesema sio mbaya kwa mtu mwenye uwezo kurekebisha kitu kwenye mwili wake huku akisema kuwa ana lenga kutumia shillingi millioni 2 za Kenya kuongeza makalio yake.
Syokau amesema amechukua hatua hiyo kwa ajili ya kuwavutia wanaume wengi ambao atawahubiria neno la Mungu ili waweze kubadili mienendo yao na kukumbatia uwokovu.
Lakini pia ameweka wazi mpango kupunguza tumbo kwenye mwili wake kwa kuwa vitambi vinasumbua sana wadada, hivyo hata yeye akipata pesa zake ataenda kukitoa.