Msanii wa Bongofleva Juma Jux amefunguka kupungua sana kimwili baada ya mashabiki kuzungumza mengi juu ya muonekano wake.
Jux amesema kuwa sababu kubwa ya yeye kukonda ni kukosa muda wa kupumzika, kula na kutofanya mazoezi kutokana na albam yeke aliyokuwa akiiandaa kwa mashabiki zake alikosa muda mzuri ndio maana amepungua.
Msanii huyo amewahakikishia mashabiki zake kuwa, mwili wake siku si nyingi utarudi katika hali ya kawanda kwani, anatarajia kuanza tena kufanya mzaoezi ili aweze kurudisha mwili.
Lakini pia amesema kuwa hashindani na msanii yoyote bali anafanya muziki kwa ajili ya nchi na mashabiki zake na ndio maana kwenye album yake itwayo King Of Heart hajashirikisha wasanii wakubwa.