Mwanamuziki wa Bongofleva, Juma Jux amefunguka na kudai kwamba hana uhusiano wowote wa kimapenzi na mrembo Huddah kutoka nchini Kenya.
Kwa kipindi kirefu kumekuwepo na tetesi za wawili kuwa pamoja ila sasa zimepamba moto baada ya Huddah kutokea kwenye video ya Jux, Simuachi.
“Tufanye kwa ufupi ni rafiki yangu, nje ya vile ambavyo watu wanamjua, ni mtu ambaye anafikiria kitu ambacho kinaweza kutunufaisha wote wawili kila tunapokutana, kama umeona video kuna product zake kule,” Jux ameimbia The Switch ya Wasafi FM.
Hata hivyo amekanusha kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake, mrembo Jackie Cliff akisema hajawahi kuonana na mrembo huyo tangu atokea jela na kurejea nchini Tanzania kwani tayari ana mtu wake.
“Niwe muwazi hatuna mawasiliano yoyote lakini mara ya kwanza kabisa wakati ametoka tulishawahi kuwasiliana, alinitumia tu meseji basi tukaongea” amesema juma_jux na kuongeza, “Kwa hiyo sasa hivi nadhani kitu kizuri ametoka ana uhuru wake kama kawaida hicho ndio kitu muhimu, mimi na maisha yangu, lakini kiukweli hatuna mahusiano yoyote.”
Utakumbuka Jux amewahi kuwa na mahusiano na wanawake maarufu kama Jacqueline Wolper, Jackie Cliff na Vanessa Mdee.