Mwanamuziki kutoka lebo ya 001 Music K.O ameachia rasmi EP yake mpya inayokwenda kwa jina la Form nne EP.
Form nne EP ina jumla ya ngoma nne za moto na bonus track mbili ambapo amewashirikisha wakali kama Susumila, Slyvia Ssaru,Tundaman, na wengine kibao.
EP hiyo ina ngoma kama Soba, Waonyeshe akiwa na Sylivia Ssaru,Ngoja akiwa na Tundaman pamoja na Dully Sykess, na Akathope huku bonus tracks zikiwa ni Nimempata akiwa amemshirikisha Susumila na Nitakoma akiwa wanafunzi wa shule ya upili ya Shimo la tewa
Form nne EP ni Kazi ya kwanza kwa mtu mzima K.O tangu aanze safari yake ya muziki na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mtandao wa kukisikiliza na kupakua muziki wa Boomplay Kenya.