Rapa kutoka Kenya Kaa La Moto ameachia rasmi Album yake mpya, inayokwenda kwa jina la “Mkanda Mweusi.”
Album hiyo, ina jumla ya mikwaju 15 huku ndani akiwapa shavu wakali kama AY, Joh Makini, Dully Sykes, Kala Jeremiah, Johnny Skani, Jua Cali, Kelechi Africana na wengine wengi.
Hata hivyo Mkanda Mweusi Album inapatikana Exclusive kwenye majukwaa yote ya kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni.
Hii itakuwa ni album ya pili kutoka kwake mwaka huu ikizingatiwa kuwa mwezi Mei aliachia Album iitwayo “Leso ya Mekatilili” iliyokuwa na jumla ya nyimbo 12.