Rapa kutoka Kenya Kaa La Moto ameachia Tracklist ya Album yake mpya, inayokwenda kwa jina la Mkanda Mweusi.
Album hiyo, ina jumla ya mikwaju 15 huku ndani akiwapa shavu wakali kama AY, Joh Makini, Dully Sykes, Kala Jeremiah, Johnny Skani, Jua Cali, Kelechi Africana na wengine wengi.
Hata hivyo amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kupokea Mkanda Mweusi Album, ambayo itaingia sokoni rasmi Disemba 20 mwaka huu.
Hii itakuwa ni album ya pili kutoka kwa mtu mzima Kaa La Moto kwa mwaka huu ikizingatiwa kuwa mwezi mei mwaka huu aliachia Album iitwayo Leso ya Mekatilili iliyokuwa na jumla ya nyimbo 12.