Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Kabako anakadiria hasara ya maelfu ya pesa baada ya kusitisha onesho lake huko Kyenjonjo kutokana na kushindwa kutumiza maagizo aliyopewa na polisi.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Kabako amesema polisi walimkatishia tamaa baada ya kumtoza pesa nyingi ili wampe ruhusa ya kuandaa onesho hilo, jambo ambalo amedai lilikuwa nje ya uwezo wake kwani angeweza kumudu gharama hiyo.
Msanii huyo amewaomba radhi mashabiki zake kwa kukosa kuandaa show yake kama ilivyoratibiwa huku akisema kwamba amefilisika kiuchumi kwa sababu alitumia pesa nyingi kuwalipa wasanii na kuipigia ubatu onesho lake hilo ambalo amelisitisha baada ya kupata vikwazo kutoka kwa polisi.
Hata hivyo Kabako ambaye ameonekana kuumizwa na kitendo cha kusitisha show yake ametoa wito kwa maafisa wa usalama nchini Uganda kufanya mageuzi kwenye baadhi ya sera zao kwani zimekuwa kizingiti kwa wasanii kuandaa matamasha yao ya muziki kutokana na polisi kuwatoza pesa nyingi wanapotaka kuwapaa vibali.