Msanii Kalifah Aganaga amedai kwamba wasanii wa Uganda hawana uwezo wa kushinda kisanaa na wenzao kutoka Nigeria.
Bosi huyo wa Bad Character Records amesema tasnia ya muziki nchini humo imekosa wawekezaji wa kuupeleka muziki wao kwenye soko la kimataifa.
Aganaga amesisitiza kuwa nchi ya Nigeria ina wawekezaji wengi ambao wanatumia mabillioni ya fedha kutanua wigo wa wasanii wao kutambulika kimataifa.
Kauli ya Kalifah Aganaga inakuja baada ya baadhi ya wasanii kutoa lalama zao kwa serikali kuweka mikakati ya kuwashinikiza mapromota wa muziki kuwapa kipau mbele wasanii wa ndani kwenye matamasha yao ya muziki tofauti na wasanii wa kigeni.