You are currently viewing KALIFAH AGANAGA AMCHANA PRODYUZA DADDY ANDRE,ADAI HANA VIGEZO VYA KUWA KIONGOZI

KALIFAH AGANAGA AMCHANA PRODYUZA DADDY ANDRE,ADAI HANA VIGEZO VYA KUWA KIONGOZI

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Kalifah Aganagah amemtolea uvivu prodyuza Daddy Andrea kwa kusema kwamba hana vigezo vya kuwa naibu wa rais wa muungano wa wasanii nchini chini humo.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Aganaga anadai Daddy Andre alishindwa kudhibiti mahusiano yake ya kimapenzi, hivyo sio mtu wa kuaminika kwenye masuala ya kuongoza wasanii wa uganda kupitia muungano wao.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Kiboko” ametoa kauli hiyo ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu Daddy Andre avunje uhusiano wake na Nina Roz baada ya prodyuza huyo kujitambulisha kwa wazazi wa Nina Roz kama mume wake.

Kalifah Aganaga na Daddy Andre wanatarajiwa kichuana vikali kwenye kinyanganyiro cha unaibu wa rais wa muungano wa wasanii nchini Uganda katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke