You are currently viewing KALIFAH AGANAGA AMSHAURI PRODYUZA WA MUZIKI DADDY ANDRE AACHE KUIMBA

KALIFAH AGANAGA AMSHAURI PRODYUZA WA MUZIKI DADDY ANDRE AACHE KUIMBA

Mwanamuziki na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Uganda Khalifah Aganaga amemtaka Daddy Andre kuamua iwapo anataka kuwa mtayarishaji wa muziki au mwimbaji.

Kulingana na Aganaga, ni vigumu msanii kufanikiwa kwenye nyanja mbili za utayarishaji wa muziki na uimbaji kwa wakati mmoja.

Hitmaker huyo wa “Kiboko”  amesema ikiwa daddy andre ataendelea kuimba atapoteza biashara kama prodyuza ikizingatiwa kuwa wasanii watamkimbia kwa hofu ya kuibiwa ubunifu wao kwenye nyimbo zao.

“Ikiwa ataendelea kuimba, atapoteza biashara yake kama prodyuza. Baadhi ya wanamuziki wakubwa na wenye vipaji watamkimbia wakihofia kuwa anaweza kuiba mawazo yao na kuyatumia kwa manufaa yake,” Aganaga alisema kwenye mahojiano.

Hata hivyo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa prodyuza anayeimba hawezi tenga muda kwa wasanii wanaotaka kufanya kazi nae kwani atajikita zaidi kwenye muziki.

“Prodyuza anayeimba hawezi tenga muda kwa msanii mwingine. Producer atajikita zaidi kwenye muziki wake kuliko watu anaofanya nao kazi,” aliongeza.

Mpaka sasa Daddy Andre hajazungumza chochote kuhusiana na vijembe vya Kalifah Aganaga.

Daddy Andre ana nyimbo nyingi kwenye kabati la muziki wake ikiwemo; “Tugende Mu Church”, “I miss you” “Omwana wa Bandi”, “Hurt you” miongoni mwa zingine.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke