Mapema wiki iliyopita msanii kutoka nchini Uganda Kalifah Aganaga alipewa ufadhili wa masomo katika Chuo Kikuu cha Victoria ambapo alitakiwa ajiandikishe kwa ajili ya kusomea kosi ya usimamizi wa matamasha na Mauzo ya Kidijitali kwa maana ya digital marketing and Events Management.
Baada ya kupewa ofa hiyo Kalifah Aganaga amedai kwamba hana haja na ufadhili huo wa rais Yoweri Museveni.
Hitmaker huyo wa “Kiboko” awali alitaka kusomea uhandisi wa sauti nchini Marekani lakini serikali ya Uganda haikufanisha suala la kumfadhili msanii huyo kusomea kozi hiyo.
Itakumbukwe mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu alimsuta vikali Rais Yoweri Museveni kwa madai ya kushindwa kutimiza ahadi yake aliyotoa ya kumfadhili kusomea kozi ya uhandisi wa sauti nchini Marekani.