Mwanamuziki wa Dancehall kutoka nchini Uganda Kalifah Aganaga amedai kwamba mapromota wa muziki nchini humo hawana nia njema ya kuupeleka muziki wa Uganda kimataifa.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Aganaga amesema mapromota wengi nchini Uganda hawataki kuwapa wasanii wa ndani kipau mbele kwenye matamasha yao ya muziki na badala yake wamekuwa wakiwazingatia sana wasanii wa Nigeria, jambo ambalo amedai sio sahihi kwani wasanii wa ndani wana ushawishi mkubwa kuliko wa nje.
Bosi huyo wa lebo ya muziki ya “Bad Character Records” ameenda mbali zaidi na kusema kwamba mapromota wa muziki nchini Uganda hawajawahi watakia mema wasanii wa muziki nchini humo ikizingatiwa kuwa wengi wao ni wanafiki.
Utakumbuka katika siku za hivi karibuni wasanii wa Nigeria wamekuwa wakitumbuiza sana kwenye shows mbali mbali nchini Uganda tangu Rais Yoweri Museveni afungue uchumi wa nchi hiyo ambapo tayari tumewaona wasanii kama Ruger na Chike wakifanya shows zao huku wasanii kama Tiwa Savage,FireBoy na Burna Boy wakitarajiwa pia kutumbuiza kwenye shows zao.